Sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi yaanza kutumika

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametangaza kuwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2023 imeanza kutumika Mei Mosi mwaka huu.

Sheria hiyo iliyopigiwa chapuo na wanaharakati wa masuala ya haki za binadamu ilisainiwa na Rais Samia Suluhu Hassan Januari 31, 2023 na sasa taarifa binafsi za watu zitalindwa kwa sheria.

Sheria hiyo imeanzisha vitu vitatu; Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi, bodi ya masuala ya taarifa binafsi na ulinzi wa faragha ya watu.

Tangazo la Waziri wa Habari halikuweka wazi ikiwa Serikali tayari imeshaunda Bodi na Kuteua Mkurugenzi wa Tume ambaye atakuwa anafanya kazi za kila siku.

“Mkurugenzi atakuwa na sekretarieti, au watumishi, ambao kazi yao ukisoma hii sheria imelazimisha wakusanya taarifa wote – hapa tunazungumzia makampuni ya simu, tunazungumzia mahospitali, tunazungumzia vyuo vikuu, labda maofisi kama ya kwetu – lazima wa
sajiliwe na hii tume,” amesema Wakili Benedict Ishabakaki katika mahojiano na Waandishi wa Habari.

“Kwamba lazima uende ujisalimishe kwamba mimi ni mmoja wa wakusanya taarifa za watu ili uweze kusajiliwa. Lakini pia baada ya hapo sheria imetoa majukumu mbalimbali. …Kwa sheria hii sasa imenyima kutoa taarifa za Mtanzania yoyote nje ya nchi bila aidha ya ridhaa ya tume ama bila ya ridhaa ya mtu husika.”

Habari Zifananazo

Back to top button