Shibula yaifunga Bugogwa ‘Angeline Cup’
TIMU ya kata ya Shibula imeanza vizuri mashindano ya The Angeline Jimbo cup baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bugogwa katika mchezo wa kundi D uliochezwa leo katika uwanja wa shule ya msingi Bugogwa.
Mpaka mapumziko timu hizo ziltoka bila ya kufungana lakini timu ya Bugogwa ilikuwa imetawala mchezo huo na kupoteza nafasi nyingi
Bao la Shibula lilifungwa na Awadh Murutemwanga kwa mkwaju wa penati dakika ya 55.
Shibula inatarajiwa kucheza tena Alhamis dhidi ya Sangabuye huku Bugogwa itacheza na Kayenze siku ya Jumatano. Kwa ushindi wa leo Shibula inaongoza kundi D ikiwa na pointi Tatu.
Katika mchezo wa kesho wa kundi D,Kata ya Sangabuye itacheza dhidi ya Kayenze katika uwanja wa shule ya msingi Bugogwa.