Shigela awafariji wachimbaji wadogo

Atoa maagizo kwa DC na timu yake

GEITA: MKUU wa Mkoa wa Geita, Martin Shigella ametembelea mgodi wa Kanegere uliopo wilayani Mbogwe na kuwafariji  wachimbaji wadogo baada ya hivi karibuni  kuangukiwa na kifusi wakiwa kwenye harakati za uchimbaji.
Watu wawili walipoteza maisha na wengine zaidi ya 20 kufanikiwa kutoka wakiwa salama.
Pamoja na mambo mengine, Mkuu wa Mkoa amewapa pole wachimbaji hao wadogo lakini pia kuwashukuru kwa namna ambavyo wametoa ushirikiano kwa uongozi wa Wilaya katika kuhakikisha kuwa sehemu hiyo ya mgodi uliosababisha maafa unasitishwa kwa muda hadi muafaka wa mgogoro ulipo baina ya mmiliki wa leseni na mwenye shamba utakapotatuliwa.
“Niwapongeze  viongozi wa Wilaya ya Mbogwe kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi ili kuhakikisha usalama wa wananchi unawekwa mbele zaidi.” Amesema Shigela
Aidha, katika ziara hiyo, Shigela pia ametembelea eneo linalojengwa mradi wa Shule ya Sekondari iliyopo katika Kata ya Nyakafulu wilayani Mbogwe na kuwataka wakandarasi waliopewa kazi hiyo kuhakikisha wanaimaliza ndani ya muda uliopangwa.
Pia, ameuagiza  uongozi wa Wilaya ya Mbogwe kusimamia kwa karibu   mradi huo ambapo zaidi ya sh mil 400 zimetolewa na Rais Samia kukamilisha ujenzi wa shule hiyo muhimu kwa wananchi wa Kata ya Nyakafulu na Wilaya ya Mbogwe kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Sakina Jumanne Mohamed amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa uongozi wa Wilaya utaendelea kusimamia kwa ukaribu miradi yote ambayo serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia imetoa fedha ili yakamilike kwa wakati na kwa ubora uliopangwa.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button