Shigela awatolea uvivu wazazi utoro wa wanafunzi

awapa mbinu za kuongeza ufaulu

GEITA: WANANCHI wa Mkoa wa Geita hususani wilayani Mbogwe wametakiwa kuwapeleka watoto katika shule za mchepuo wa Kingereza ili kuwajengea msingi mzuri katika safari yao ya kielimu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani Mbogwe.

Akiwa katika shule ya msingi  Nyakasaluma ambayo serikali imetoa jumla ya Sh milioni 600  amewataka kuhakikisha mradi huo wa kipekee wa shule ya msingi ya serikali ya mchepuo wa Kiingereza “English medium”, unatekelezwa

“Shule ipo nzuri tu,  wananchi waleteni watoto  pindi usajili wa wanafunzi utakapoanza.” amesema

Aidha, Shigela amewahimiza wananchi kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili serikali inapoleta fedha, wananchi wasihangaike kutafuta maeneo.

Kauli ya Shigela imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Sakina Mohamed kudai kuwepo kwa mdondoko wa elimu wilayani humu na kwamba zaidi ya wanafunzi 200 walioandikishwa kufanya mitihani ya darasa la nne hawakutokea kufanya mitihani hiyo.

Amesema hali hiyo inachangiwa na wazazi kutowahimiza watoto kwenda shule badala yake wanawatumia kwenye shughuli zao za kibiashara.

“Wazazi wanachangia mdondoko wa shule kwa watoto wao, wanawatuma kwenye biashara zingine zisizo rasmi kama uuzaji wa mafuta kiholela barabarani.” amesema

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button