Shigongo Cup kuibua vipaji

TIMU 22 kati 21 za Jimbo la Buchosa Wilaya Sengerema mkoani Mwanza zinatarajia kumenyana kusaka vipaji kwa vijana wa jimbo hilo kwenye michuano ya Shigongo Cup inayotarajiaa kuanza Julai 26 mwaka huu.

Kuelekea michuano hiyo, Mbunge Eric Shigongo amegawa vifaa vya michezo kwa timu zote zitakazoshiriki mashindano hayo ambazo ni  jezi, mipira na ‘track suit’ vyenye thamani ya Sh million 16.

Advertisement

“Buchosa inavijana wengi wenye vipaji vya kucheza soka  hivyo tumeamua kuviibua na kuvionesha wa timu kubwa za simba,yanga,azam na timu nyingine za ligi kuu,ligi daraja la kwanza,daraja la pili na hata kuonekana  kwenda kucheza soka nje ya Tanzania.”Alisema

Mratibu wa mashindano hayo, Marco Zakalo amesema mashindano hayo yana historia kubwa kwani imewaibua nyota wengi kama Mrisho khalfan Ngasa, Kennedy Juma wa Simba, Sebusebu Samsoni kipa wa Geita Gold na wachezaji wengine wengi waliopita katika mashindano hayo.

Diwani wa kata ya Bupandwa Masumbuko Bupamba amesema kuanzishwa kwa ligi hiyo kutaitangaza vyema Buchosa kwani itasaidi  kuibua vipaji ambavyo havijapata jukwaa la kuonekana huku akiwaomba vijana na mashabiki kujitokeze kwa wingi kufuatilia mashindano hayo.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *