Shigongo: Sheria ilinde Watanzania

MBUNGE wa Buchosa, Eric Shigongo amesema sheria zinazotungwa lazima ziwalinde Watanzania, vinginevyo kutakuwa na kulaumiana na kufilisika kwani wanalazimika kuingia katika ushindani ambao hawataumudu.

Ametoa kauli hiyo leo Septemba 7, 2023 alipokuwa akichangia hoja kwenye Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023, uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba.

Amesema kama sheria haitalinda Watanzania, viwanda vitakufa na kusistiza kuwa kila nchi duniani inalinda watu wake kisheria na kuwasiadia kukua kiuchumi.

“Sipingi uwekezaji ila lazima tuwalinde watu wetu waweza kushindana kukua,” amesema Mbunge huyo.

Hata hivyo Mbunge huyo amesema hana amani kutokana na Ibara ya 57 ya muswada huo kwa sababu inaleza endapo rasilimali fedha zimetolewa na serikali pekee itatengwa fedha kwa ajili ya viwanda vya ndani ambazo ni Sh bilioni tano.

Amesema kutokana na hali hiyo, Mtanzania akiomba zabuni yenye zaidi ya Sh bilioni tano atashindana na washindani wa nje, hivyo kuna haja ya kuweka mazingira ya kumlinda Mtanzania na kushauri kiwango hicho kiwe angalau Sh bilioni 50 kwa washindani wa nje.

Akifanya majumuisho ya hoja mbalimbali za wabunge, Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, amesema wamekubaliana na wazo la Mbunge Shigongo pamoja na Kamati ya Bajeti kuwa tenda ya kimataifa iwe kuanzia Sh bilioni 50.

Amesema ni nia ya serikali kuwapa fursa Watanzania kuwawezesha na kuwafanya wakue kiuchumi.

Habari Zifananazo

8 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button