Shilole: Mwijaku amuombe radhi Khadija Kopa

DAR ES SALAAM: Msanii wa Bongo Fleva nchini Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amemtaka Burton Mwemba ‘Mwijaku’ amuombe radhi mwimbaji na malkia wa muziki wa taarab nchini, Khadija Kopa baada ya kutupiana maneno hivi karibuni katika mitandao ya kijamii.

Shishi ameandika kwenye instagram yake; “Mama Khadija ni mwanamuziki ambae mimi nimeanza kumsikia toka mdogo kwetu Igunga mpaka leo mimi ni msanii.

“Ni mama ambae sisi wanamuziki wa kike tuna muangalia na kutamani uwezo alionao toka msichana mpaka leo mama na wajukuu”.

“Kiukweli unapo mkosea heshima huyu mama ni sawa na kutukosea heshima wanawake na sio wanawake tu bali Hata Mila na tamaduni zetu zimetuasa kuheshimu wakubwa. Sijpenda ulichofanya ndugu yangu Mwijaku naomba umuombe radhi mama Khadija Kopa”.

Habari Zifananazo

Back to top button