MSANII wa bongo fleva Zuwena Mohammed, ‘Shilole’ amesema anatafuta mbinu mpya ya kupunguza mwili kwani mazoezi yamemshinda.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole amesema kuwa amefanya mazoezi vya kutosha na hapungui anataka mbinu mpya.
“Nimefanya mazoezi vya kutosha sasa naona sipungui, nipo kwenye kula kwa mpangilio, nikitafuta mbinu mpya,”amesema Shilole
Pia ameongeza kuwa ikiwezekana ataulizia vizuri kuhusu puto kama aliloweka msanii Peter Msechu.
Comments are closed.