Msanii wa muziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamed maarufu ‘Shilole’ amewataka wanawake wawalinde watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na matumizi ya mitandao ya kijamii.
Shilole amesema hayo leo Machi 5, 2023 wakati akizungumza na wanawake wa Wilaya ya Pangani ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani.
Amesema wanawake ndio wana jukumu kubwa la malezi kwa watoto wao, hivyo wawalinde dhidi ya vitendo vya ukatili pamoja na utandawazi uliopo kwenye mitandao ya jamii.
“Kuna ukatili mkubwa kwenye mitandao ya kijamii hivyo walindeni watoto wenu wasiharibike, kwani Taifa linawategemea,”amesema Shilole