Shiloow mwenyekiti ALAT Tanga

MSTAHIKI Meya wa Jiji la Tanga, Al-Hajj Abdulrahman O.

Shiloow amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania (Association of Local Authorities of Tanzania – ALAT) Tawi la Mkoa wa Tanga, katika uchaguzi uliofanyika leo.

Hatua hiyo ni baada ya kujiuzulu hivi kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe Vijijini, Sadick Kallaghe.

Katika mkutano huo wa uchaguzi, ambao wajumbe wake ni Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri ndani ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Madiwani wawili kutoka kila Halmashauri ndani ya Mkoa, walimchagua Meya Shiloow kwa kura 24 dhidi ya kura 15 alizopata mpinzani wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilindi, Idrisa Mgaza.

Jumuiya ya Tawala za Serikali za Mitaa Tanzania Bara (ALAT), ni Jumuiya ya Halmashauri zote za Wilaya, Majiji, Manispaa, Miji Midogo na Vijiji, ambayo ilianzishwa mwaka 1984 baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa Serikali za Mitaa

Habari Zifananazo

Back to top button