MASHINDANO ya Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (Shimiwi) yameendelea kushika kasi mkoani Tanga.
Katika michezo iliyofanyika leo, timu ya netiboli ya Bunge iliifunga Tarura mabao 16-11, wakati mpira wa miguu Bunge na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.