Shuhuda wa ajali ya Precision Air: Nilitamani kuandika barua

Zhang Lin, Manusura ajali ya Precision Air

ZIKIWA zimepita siku nane tangu kutokea kwa ajali ya ndege ya ‘Precison Air’ katika Ziwa Victoria na kuuwa watu 19, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Zhang Lin alikuwa miongoni mwa watu 43 waliokuwa kwenye ndege hiyo.

Katika Mahojiano na HabariLEO, Zhang Lin ambaye ni raia wa kigeni anasimulia kuwa mara baada ya ndege hiyo kupaa; alipitiwa na usingizi kutokana na uchovu kwani aliamka mapema sana kujiandaa na safari yake.

Lin anasema alikuwa amesinzia muda wote tangu ndege ilivyoanza safari. aliamka saa mbili asubuhi dakika 30 kabla ya ndege kuanguka. Alikuwa amekaribia kufika. Anasema amekuwa Bukoba akiwa Mhandisi wa Ujenzi akishirikiana na Kampuni ya China Communications Construction Company Limited (CCCC).

Advertisement

“Nilichungulia dirishani, kulikuwa na radi. Hali ya hewa ilikuwa mbaya sana. Hadi nilipoona kwamba ndege ilikuwa inakaribia zaidi ziwa, nilijua kwamba ndege ilikuwa karibu kutua ziwani…,” anasema Zhang Lin, mmoja wa manusura 24 wa ajali mbaya ya ndege.

CCCC inatekeleza moja ya miradi mkoani Kagera. Anakumbuka kwamba, “nilipochungulia dirishani niliona radi, hali ya hewa ilikuwa mbaya na ndege ilikuwa inakaribia ziwa.”

Anasema alifahamu kuwa ndege hiyo ilikuwa inakaribia kutua “Nilijua kwamba ndege ilikuwa karibu kutua. Kwa uzoefu wangu, ilikuwa hatari kutua katika hali mbaya ya hewa, kwa hiyo nilishika kiti cha mbele kwa mikono yangu. Nikijiweke tayari kwa ajali,” anasema Lin.

 

Mabaki ya Ndege ya Precision Air

Lin anafafanua zaidi kwamba, muda mfupi baadaye, alisikia kishindo kikubwa na miguu yake kugongwa kwenye kiti cha mbele. Lin anasema kukaa kwake kiti cha nyuma kulisaidia kutopata majeraha makubwa. Akiwa bado katika mshtuko Lin aliona sehemu ya mbele ya ndege ikiwa imefurika maji.

“Mara moja nilitoa jaketi la kuokoa maisha, nikalivaa, nikafungua mkanda na kusimama. Mlango ulikuwa bado umefungwa, kwa hiyo nilipiga kelele ‘kufungua mlango na kiwango cha maji kiliongezeka kwa kasi sana. Nilihisi nilikuwa nakaribia kifo.” Lin anaendelea kutoa ushuhuda.

Kutokana na hali hiyo ya kutokuwa na uhakika, Lin alifikiria kuandika barua kwa familia yake lakini hakukuwa na wakati wa kufanya hivyo.

“Ghafla, nikaona mwanga ukiingia mlangoni sikuwa na uhakika na nani alifungua mlango kisha nikafungua mlango kabisa na abiria wengine wachache na nikaogelea kutoka ndani ya ndege nikiwa na koti langu la kuokoa maisha.” anaongeza Lin.

Alisimulia kwamba alipotazama nyuma, alimuona mtoto akiwa ameinuliwa hewani karibu na mlango, hakufikiria mara mbili na mara akapanda ubawa ili kumuokoa mtoto huyo.

“Nilifanikiwa kufika kwenye mkia wa ndege na kumchukua mtoto kutoka kwa mtu ambaye pia alihitaji kuokolewa. Nikiwa nimemshika mtoto huyu kwa uangalifu, nilirudi kwenye bawa, na punde si punde wavuvi walikuja kuniokoa. Mimi na mtoto tulipelekwa kwenye gari la wagonjwa ufukweni. Tulipelekwa hospitalini na abiria wengine waliookolewa,”

Lin hata hivyo aliishukuru serikali ya Tanzania na wananchi wa Kagera kwa jitihada zao za kuokoa maisha yake na ya abiria wengine.

1 comments

Comments are closed.