Shule 33 Ilemela kupatiwa madawati

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imekabidhi madawati 710 kwa shule 33 za msingi katika manispaa hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo yaliofanyika leo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala ameishukuru halmashauri kwa kutoa madawati hayo.

Amesema madawati hayo yamegharimu zaidi ya Sh milioni 100 na kwamba katika madawati hayo, Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela ilichangia Sh milioni 32 na wadau mbalimbali walichangia Sh milioni 72.

‘’Lengo letu kwa sasa ni kumaliza tatizo la madawati na tunashukuru wananchi na wadau mbalimbali, waliotusaidia na wanaoendelea kutusaidia katika utoaji huu wa madawati,’’ amesema Masala.

Amesema katika awamu ya kwanza walifanikiwa kutoa madawati 431 kwa shule 21 za msingi.

Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Modest Apolinary amewashukuru wadau mbalimbali waliochangia na kwamba haikuwa kazi rahisi na kupongeza juhudi za Mkuu wa Wilaya ya Ilemela kuhamasisha upatikanaji wa madawati hayo.

Habari Zifananazo

Back to top button