Shule ya Sekondari ya wasichana Longido kuanza kazi Februari

ARUSHA: Mkuu wa Mkoa Arusha,John Mongella amesema hadi kufikia Februari 01, 2024, shule mpya ya Sekondari iliyopewa jina la” Longido Samia Girl’s Sekondari” ya masomo ya Sayansi itaanza kutoa elimu ili kuwezesha watoto jamii ya wafugaji kusoma na kupata wasomi wengi nchini wanaoweza kujiajiri wenyewe.

Rc Mongella amesema hayo wilayani Longido wakati wa ukaguzi wa shule hiyo ya Samia Girls Sekondari inayojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh,bilioni 3 ikiwa na lengo la kuleta mapinduzi makubwa ya elimu kwa jamii hiyo.

“Shule hii majengo yake baadhi yamekamilika na mengine yanaendelea kujengwa ila hapa ni lazima fundi wa aluminum na magrili aweke kambi hapa kwaaajili kufitisha madirisha hapa lazima tuongeze nguvu kutoka mkoani ili shule hii ikamilike Februari mosi mwaka huu na wanafunzi waanze kusoma”

Amesema kwenye maeneo ya wafugaji kunachangamoto kubwa ya kutowapa vipaumbele watoto wa kike hivyo Rais Samia Hassan Suluhu ameamua kuondoa dhana hizo potofu kwa kujengwa shule hiyo ya mfano ambayo ni kwaaajili ya wasichana pekee.

Licha ya changamoto za hapa na pale zilizopelekea kuchelewa kukamilika kwake kasi ya ujenzi inaendelea zaidi ili kuhakikisha majengo zaidi ya 20 yanayoendelea kujengwa yanaisha na kukamilika kwa ubora unaotakiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button