Shule yafafanua mbinu za ufaulishaji

SHULE ya sekondari Kiuta iliyopo Halmashauri ya Mji wa Newala mkoani Mtwara imekuwa ikifanya vizuri matokeo ya kidato cha sita kutokana na jitihada mbalimbali za ufundishaji wanazotumia walimu shuleni hapo.

Akizungumza wiki hii kwenye halmashauri hiyo, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Jane Mlelwa amesema mafanikio hayo yanatokana na mbinu mbalimbali ikiwemo ufuatiliaji wa ufundishaji darasani, mitihani ya mara kwa mara.

Matokeo ya kidato hicho mwaka 2023, daraja la kwanza wamefaulisha wanafunzi 94, la pili 25 na la tatu 1 kati ya wanafunzi 120 waliofanya mtihani mwaka huo.

Matokeo hayo yamepelekea shule hiyo kushika nafasi ya 3 kimkoa, kitaifa 75 kati ya shule 684 za kata nchini.

Aidha, mwaka 2021/22 ilikuwa na watahiniwa wa kidato cha sita 115 waliyofanya mtihani wa taifa wakapat daraja la kwanza 32, la pili 81 na la tatu 2.

licha ya kuwepo kwa mafanikio hayo ila inakabiliwa na baadhi ya changamoto ikiwemo uzio hali itayohatarisha usalama wa wanafunzi waishio shuleni hapo.

Ofisa elimu sekondari wa halmashauri hiyo, Athumani Salum amesema wamejiwekea mikakati ya kuhakikisha walimu wanafundisha vizuri, ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kubaini kama walimu wanafundisha kupitia matokeo ya Wanafunzi.

Mwanafunzi wa kidato cha sita shuleni hapo, Elizabert Francis ‘’Kupitia elimu bure inayotolewa na serikali imetuwezesha sisi wanafunzi wa kike kusoma bila kikwazo chochote”,amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button