Shule za msingi Mtwara zagaiwa mipira kukuza vipaji

CHAMA cha Mpira wa Miguu mkoani Mtwara (MTWAREFA) kimekabidhi mipira 1,000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas.

Mipira hiyo imetoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kugawa katika shule za msingi ili waweze kuibua vipaji, zoezi ambalo limefanyika leo Machi 7, 2024.

Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa mkoa wa Mtwara, Athumani Kambi amesema mipira hiyo wamepewa na kuagizwa igaiwe katika halmashauri zote tisa kwenye mkoa huo.

‘’Niimize ofisa michezo, walimu wa shule, mwenyekiti wa vyama vya michezo na makatibu wake wafuatilie mipira inapokwenda na pia TFF watafuatilia”

Mkuu huyo wa mkoa, ameishukuru TFF kwa kuhakikisha wanainua viwango vya mchezo wa mpira wa miguu mkoani humo.

‘’Naomba kusisitiza kwenye halmashauri na wilaya waongeze jitihada za kuwajengea uwezo vijana hawa na vipaji vipo kinachotakiwa ni kufanya mashindano kuanzia ngazi za chini,” amesema Abbas

Kaimu Ofisa Utamuduni, Sanaa na Mchezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Shadya Namkoko amesema tukio la upokeaji wa vifaa hivyo limempa nguvu ya kusimamia vijana kwenye michezo.

Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Rahaleo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani humo, Jackson Ogo ameishukuru TFF kwa kuleta mipira hiyo kwa kuwa shule yao ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya mipira.

“Tunaamini mipira hii itaenda kukuza vipaji shuleni kwetu na kinua vijana watakaocheza katika timu ya taifa hapo baadaye”

Habari Zifananazo

Back to top button