Shule Zambia zafunguliwa

SHULE nchini Zambia zimefunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka huu, baada ya kuchelewa mara kadhaa kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Kufunguliwa kwa shule kulicheleweshwa kwa wiki tano kama sehemu ya safu ya hatua za kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo unaoambukiza.

Wizara ya Elimu ilisema imekuwa ikifanya ukaguzi wa shule kote nchini ili kutathmini utayari wao wa kufunguliwa tena.

Advertisement

Kuenea kwa ugonjwa huo kumepungua, kulingana na mamlaka.

Takriban watu 500 wamefariki tangu mlipuko huo uliporipotiwa Oktoba mwaka jana. Zaidi ya kesi 15,000 hadi sasa zimeripotiwa.

Zambia imekuwa na milipuko kadhaa mikubwa ya kipindupindu lakini mlipuko wa sasa ni mbaya zaidi kuwahi kutokea katika miaka 20, kulingana na serikali.