Shule zafungwa Ufaransa kisa kunguni
SERIKALI ya Ufaransa inafanyia suala la kuzuia hofu ya kitaifa kuhusu kunguni, huku baadhi ya shule jijini Paris zikikumbwa na ghasia hiyo na kupelekea kufungwa.
Maafisa wakuu kutoka Wizara za Afya, uchumi na uchukuzi wanakutana Ijumaa katika ofisi ya Waziri Mkuu kuratibu mpango wa hatua dhidi ya wadudu hao.
Nicolas Roux de Bézieux, muundaji wa tovuti ya kudhibiti wadudu amesema katika simu tatu kati ya nne anazopokea kutoka kwa wamiliki wa nyumba matatizo yanakuwa kunguni.
Romain Morzaderc, mdhibiti wa wadudu huko Brittany, aliliambia gazeti la Ouest-France kwamba “katika asilimia 99 ya visa, kuna wadudu wabaya weusi, lakini hapana, sio kunguni”.
Serikali imeshtushwa na jinsi habari za kunguni zilivyotawala vichwa vya habari ndani na nje ya nchi. Mawaziri wanahofia taswira ya Paris inaharibiwa, na kwamba utalii unaweza kuathirika, hasa wakati wa Olimpiki ya mwakani.
Waziri wa Uchukuzi, Clément Beaune alisema Jumatano kwamba kati kunguni 50 walioripotiwa kuonekana kwenye treni za Metro na SNCF, hakuna hata mmoja aliyethibitishwa.
“Nisingependa kuona aina ya unyanyasaji wa Kifaransa ukishikilia … kama inavyofanya wakati mwingine katika nchi za Anglo-Saxon,” alisema.
“Tatizo linahitaji kuchukuliwa kwa uzito sana. Hakuna kukataa. Na hakuna hysteria.”
Katika wiki za karibuni, kampuni za kudhibiti wadudu kote Ufaransa zimeripoti ongezeko kubwa la kunguni.