Siku 331 bila kucheza mpira zamliza Neur
UJERUMANI: Golikipa wa timu ya Bayern Munich na timu ya Taifa ya ujerumani Manuel Neur ameshindwa kuzuia furaha yake baada ya kurejea uwanjani siku ya jumamosi wakati timu yake ikiishindilia Darmstadt Mabao 8-0 katika mchezo wa Bundesliga uliopigwa Uwanja wa Alliance Arena.
Neur alikuwa nje ya uwanja kwa takribani siku 331 kutokana na majeraha lakini sasa amepona na kurejea uwanjani baada ya mchezo huo Neur amesema alikuwa katika kipindi kigumu mno lakini watu wengi walikuwa nyuma yake na kumpa moyo kuwa atarejea imara zaidi.
“Huu ni wakati bora sana kwangu na sitoweza kusahau, kwa dhati kabisa ninawashukuru wote waliokuwa nami katika kipindi cha miezi 11 ambayo sikucheza mpira” na kuongeza
Kwasasa yupo tayari kuipambania nembo ya timu yake na kuipa mafanikio zaidi.