Wilaya ya Tanganyika waitikia chanjo Uviko-19

HALMASHAURI ya Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Taasisi ya Benjamini Mkapa, imefanikisha chanjo ya Uviko-19 kwa watu 32,000 ndani ya wiki moja.

Akizungumza Kijiji cha Luhafwe, sehemu iliyotengwa maalumu kwa ajili ya utoaji chanjo, Mratibu wa chanjo Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Philip Mihayo,amesema idadi hiyo imefikiwa kutokana na hamasa na mbinu shirikishi iliyotumika kuwaelimisha wananchi.

“Tulikuwa na asilimia kama 32 hivi kabla ya ujio wa wadau, taasisi ya Benjamini Mkapa imekuja kutupa hamasa kubwa kwa sababu tumetumia mbinu ya kuwaita viongozi wa dini, viongozi wa jamii, watu wa tiba asili, tumeshirikisha watu maarufu kwa sasa hivi mwitikio ni mkubwa sana,”amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Shaban Juma, leo Oktoba 31,2022 amefika kujionea kazi hiyo inavyoenelea, ambapo ameridhishwa na mwitikio wa wananchi, huku akiishukuru taasisi hiyo kwa kujumuika nao kuhamasisha.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Dk Alex Mrema, amesema chanjo inayotolewa ni aina ya Jensen ambayo ni ya dozi moja na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika inatarajia kuwafikia wananchi 150,000.

Ofisa miradi kutoka taasisi ya Benjamini Mkapa, Zawadi Dakika, amesema sababu za kuleta mradi huo Mkoa wa Katavi ni kutokana na kuwa miongoni mwa mikoa iliyo nyuma kwa uchanjaji kutokana na hamasa kuwa chini.

Amesema kabla kampeni haijaanza Oktoba 24, 2022, Mkoa huo ulikuwa umechanja kwa asilimia 51, lakini ndani ya siku saba baada ya zoezi hilo kuanza Mkoa umefikia asilimia 85 ya uchanjaji.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x