Siku ya Shampeni yanoga Dar

OKTOBA 29,  ilikuwa Siku ya Shampeni na dunia iliadhimisha  siku hiyo kwa kuinua glasi ya shampeni katika sherehe zilizofanyika katika nchi nane tofauti.

Nchi hizo ni Tanzania ,Ufaransa, Morocco, Afrika Kusini, Uturuki, Nigeria,Ujerumani na Marekani

Nchini Tanzania sherehe hii ilifanyika jana Posta, Dar es salaam ambapo mgeni mwalikwa alikuwa mwanamitindo na Miss Tanzania mwaka 2005 Nancy Sumari.

Katika siku hii, shampeni ya Moet & Chandon ambayo ipo kwa zaidi ya karne mbili, ilisherehekewa  kwa namna ya kipekee kwa sherehe maalumu katika nchi husika.

Waalikwa katika sherehe hiyo walionea fahari Moët & Chandon ambayo imejidhihirisha kisifa kwa kuwaweka karibu marafiki, watu mashuhuri, na watu wenye  ushawishi mkubwa.

“Siku ya Shampeni ni fursa ya kusherehekea ubora usio na kifani kwa karibu karne tatu, ni nia ya dhati ya Moët & Chandon kushiriki furaha hiyo na dunia,” amesema Aimee Kellen, Mkuu wa Ushirikiano wa Watumiaji wa Moët Hennessy Afrika na Mashariki ya Kati.

Moet & Chandon wanasema utengenezaji mvinyo huo ni wa kipekee na wenye ubunifu wa hali ya juu ambao umesababisha kuwapo na  mapinduzi kwenye soko la kutengeneza shampeni inayotokana na mizabibu.

Moët & Chandon iliyoanzishwa mwaka 1743 ndiyo iliyochangia kutambulisha aina nyingine ya shampeni ulimwenguni kwa kutoa mvinyo wa kipekee kwa kila hafla.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x