Silaa atoa maagizo PSSF Kigoma

KIGOMA: WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amelitaka Shirika la Mafao ya Wastaafu Nchini PSSF kuacha mara moja uendelezaji wa Jengo lao katika Manispaa ya Kigoma kutokana na Shirika hilo kupewa eneo lililoifadhiwa kwa ajili ukanda wa kijani.

Waziri Silaa amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kusimamisha maendeleo yoyote ya ujenzi katika eneo hilo ikiwemo Ofisi ya Mtendaji Kata pamoja na kuondelewa kwa shughuli nyingine za kijamii na wafanyabiashara ndogondogo.

Waziri Silaa alisema hayo wakati akihitimisha ziara yake siku mbili mkoani Kigoma na kuwataka watendaji wote wa sekta ya ardhi mkoani humo kuzingatia matakwa ya sheria za ardhi ili kila mtu apewe haki yake wakati wa kufuata taratibu za kumiliki ardhi.

Waziri Silaa alisisitiza kuwa suala PSSF halihitaji hata yeye kurudi ofisini bali hataki kabisa na hivyo kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma kutoa taarifa kwa viongozi wa shirika hilo kutafuta eneo lingine hata kama linahitaji kutolewa fidia akiongeza kuwa shirika hilo ni kubwa.

Agizo la Waziri Silaa pia likawaangazia pia watu wa takwimu ambao pia wametwaa eneo bila kuwa na hati milki ya eneo husika nakuagiza waandikiwe barua ili viongozi wao wajue kuwa walinunua eneo bila kuwa na hati.

‘’Kama mmegawa eneo lililoifadhiwa kwa namna yoyote mkagawa Ofisi ya Kata, hiyo ofisi ya Kata itavunjwa alafu mtamweleza Waziri wa TAMISEMI kwanini fedha zake zimetumika kujenga katika eneo ambalo sio sahihi kwa matumizi yale ndio maana nakataa mabadiliko ya matumizi ya viwanja.’’amesema Silaa.

 

 

 

 

 

 

 

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button