Silaa: Halmashauri rejesheni mikopo ya KKK kwa wakati

MUSOMA: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Jerry Silaa amezitaka halmashauri zote zilizokopeshwa fedha za Kupanga, Kupima na Kumilikisha (KKK) Ardhi nchini kurejesha fedha hizo kwa wakati ili waweze kukopeshwa wengine.

Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wilayani Musoma Mkoa wa Mara wakati akiongea na Viongozi wa Kamati ya Usalama wa mkoa na maafisa wa sekta ya ardhi katika ziara yake ya kufuatilia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu migogoro ya vijiji 975 nchini.

Silaa amezitaka halmashauri hizo baada ya kuona halmshauri nyingi zinakopeshwa fedha hizo ambazo kazi yake ni Kupanga, Kupima na Kumilikisha viwanja kwa wananchi lakini zimekuwa hazirejeshwi kwa wakati.

Amesema, kuchelewa kurejeshwa kwa mikopo hiyo inakwamisha mzunguko wa fedha hizo ambazo wengine wanazihitaji na zinakwamisha juhudi za kuongeza mapato ya Serikali.

Aidha, amesema katika kukomesha hali hiyo wizara yake imeamua kuanzisha akaunti ya pamoja ambayo itakuwa inafanya ufuatiliaji wa fedha hizo katika matumizi na kurejeshwa kwa wakati.

 

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button