Silinde amshukuru Samia miradi ya maendeleo
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais –TAMISEMI, ambaye pia ni Mbunge wa Tunduma, David Silinde amemshukuru Rais, Dk Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo kila sekta katika Halmashauri ya Mji Tunduma mkoani Songwe.
Ameyasema hayo Tunduma katika ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika Halmashauri ya Mji Tunduma.
Amesema katika sekta ya elimu, shule maalum ya Sayansi ya Wasichana ya Mkoa wa Songwe inaendelea kujengwa eneo la Namore katika Halmashauri ya Mji Tunduma ambayo inagharimu shilingi bilioni 4.
Amesema Shule nyingine maalum moja kati ya 15 zilijengwa nchi nzima, imeshejengwa katika kata ya maporomoka ambayo imegharimu Sh bilioni 1 iliyoenda sambamba na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya kata ya Uwanjani.
Pia amesema katika miaka miwili ya Rais, Dk Samia amewezesha ujenzi wa vituo vya afya vitano katika Halmashauri ya Mji Tunduma ambavyo vitagharimu Sh bilioni 2.5.
Amesema Ujenzi wa Jengo la dharura (EMD) katika hospitali ya wilaya Tunduma linaendelea kujengwa kwa gharama ya shilingi milioni 336 na Vifaa tiba kama X-Ray na Mashine ya Kuzalisha Hewa ya Oksijeni zimeshaletwa.
Amesema bajeti ya TARURA imeongezeka kutoka Sh bilioni 1 kufikia bilioni 4 kwa sasa na ujenzi wa soko la kisasa kata ya Mazengo kwa gharama ya shilingi bilioni 2.3 pamoja na Soko la dagaa Sh bilioni 1.5