Simba bado nne kwa Yanga

IKIWA na idadi sawa ya michezo (15) Simba SC sasa imeachwa pointi nne dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Yanga wenye pointi 40 katika msimamo wa ligi hiyo.

Idadi hiyo ya pointi ni baada ya timu hiyo kushinda mchezo wake wa kiporo dhidi ya JKT Tanzania bao 1-0 Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Mbweni, Dar es Salaam leo.

Katika mchezo huo, bao la Simba lilifungwa na Clatous Chama dakika ya 36, bao lililodumu kwa dakika zote 90 za mchezo.

Advertisement

Yanga ikiwa kileleni na pointi 40, Simba wako nafasi pili wakiwa na pointi 36, Azam FC pointi 32 nafasi ya tatu wakiwa na mchezo mmoja mkononi.