WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Simai Mohammed Said ameiteua klabu ya Simba kuwa Balozi wa Utalii wa Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo leo Januari 5, 2024 imeeleza Waziri Simai amechukua uamuzi huo kwa kutambua mchango wa Simba katika kutangaza utalii wa Zanzibar na Tanzania.
Simba ilianzisha mkakati wa kuitangaza Zanzibar kupitia kauli mbiu ya Visit Zanzibar katika jezi na mitandao yake ya kijamii wakati huu wa Kombe la Mapinduzi.
“Tunaishukuru sana Serikali ya Mapinduzi wa Zanzibar kwa kutambua mchango wa timu yetu kutangaza utalii hivyo kukuza uchumi wa Zanzibar, tunaona fahari kubwa kuwa sehemu ya maendeleo makubwa Zanzibar inayoyapata.
” Ameeleza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajula.