Simba Day viwanja viwili

SIMBA wamekuja na jambo jipya bwana, wameandika barua serikalini kuomba pia watumia Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam katika tamasha lao la Simba Day Jumapili Agosti 6, 2023.

Hatua ya kuomba watumie viwanja viwili inatokana na imani yao kwamba Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ambao umepangwa kutumika kwa ajili ya tamasha hilo utakuwa umejaa mapema siku hiyo, hivyo mashabiki watakaokosa nafasi wafuatilie tamasha hilo wakiwa Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza leo Agosti 1, 2023 katika uzinduzi wa hamasa ya wiki ya Simba, Buza jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu amesema wana imani watajaza Uwanja wa Mkapa, hivyo mashabiki watakaokosa nafasi wataenda Uwanja wa Uhuru.

“Tumeandika barua kuiomba serikali itupatie na Uwanja wa Uhuru kwa kuwa tunaamini tutaujaza Uwanja wa Mkapa mapema tu,” amesema Mangungu.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button