Simba hakuna muda wa kupoteza
BAADA ya kuwasili kutoka Ivory Coast, kikosi cha Simba SC kitaingia moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy.
Kabla ya mchezo huo, Jumatano hii Simba watacheza mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya TRA kwenye uwanja wa Azam Complex.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema mpaka sasa hawajapata taarifa rasmi za ujio wa Jwaneng Galaxy na lini watawasili nchini ila watu wa maandalizi wameshawasili”. amesema Ahmed Ally.
“Mechi dhidi ya Jwaneng Galaxy itachezwa Jumamosi Machi 2, 2024 saa 1:00 usiku. Licha ya mapendekezo yetu kucheza mechi saa 10:00 jioni lakini CAF wameamua iwe saa 1:00 usiku ili michezo yote iwe muda mmoja”.amesema Ahmed Ally.