Simba hawapoi, wajifua kuikabili Al Ahly

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha Simba jana kimerejea mazoezini kujiwinda na mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Cairo International, Misri, Aprili 5.

Simba wanakabiliwa na kibarua kigumu cha kupindua meza baada ya kufungwa bao 1-0 na mabingwa hao watetezi wa kombe hilo Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Machi 29.

Wekundu hao wa Msimbazi watahitaji kupata ushindi wa zaidi ya bao moja ili kuingia hatua ya nusu fainali.

Akizungumza na HabariLEO jana, Ofisa Habari wa klabu hiyo Ahmed Ally amesema jana wameanza mazoezi na hakuna majeruhi zaidi ya Aishi Manula ambaye ali-
umia akiwa na kikosi cha Taifa Stars kwenye michuano ya Fifa Series.

“Kikosi kiko leo (jana) kimerejea mazoezini kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Ahly.

Wachezaji wote isipokuwa kipa Aisha Manula wako kwenye hali nzuri kiafya.

Tumeanza matayarisho ya mchezo huu mapema lengo likiwa kuingia nusu fainali,” amesema Ahmed.

Mara ya mwisho Simba kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ilikuwa mwaka 1974 ambapo ilifungwa na Mehalla El Kubra ya Misri kwa penalti 3-0 baada
timu kushinda mchezo wa nyumbani kwa bao 1-0.

Habari Zifananazo

Back to top button