Simba ijayo haitaki lawama na mtu

MWENYEKITI wa Bodi ya klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try again’ amesema wamejipanga kutengeneza Simba bora zaidi kuelekea msimu wa 2023/2024

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 16, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wanasimba wawe na imani na uongozi wao kwani wanawaandalia timu ya mataji msimu ujao

“Niwahakikishie Simba ijayo itakuwa Simba bora zaidi kuwahi kutoea.”

Advertisement

Aidha, ameongeza kuwa wapinzani wao wajiandae na kilio kilio msimu ujao kwani wamejidhatiti kutwaa mataji licha ya misimu miwili nyuma kutoka patupu