Simba kamili kuivaa Al-Ahly

DAR ES SALAAM: KOCHA wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema amekiandaa vizuri kikosi chake kwa mchezo wa kesho, hivyo wapo tayari kuikabili Al Ahly katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Ligi ya Soka Afrika (AFL)

Ameyasema hayo leo Oktoba 19, 2023 katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo huo, jijini Dar es Salaam.

“Mchezo wa soka kwangu ni furaha na starehe, sichukulii kama vita na nikiwa kama mwalimu wa mchezo huu, sipaswi kuwa naongea sana. Jambo la muhimu ni kuwa dakika 90 zitaamua,” amesema Robertinho.


Akizungumzia kikosi chake, Robertinho amesema barani Afrika hajaona mlinzi bora wa kati kumzidi Henock Inonga na pacha yao na Che Malone Fondoh anaihusudu kuelekea mchezo wa kesho.

Alipoulizwa juu ya uwezekano kwa mlinda lango wa klabu hiyo, Aishi Manula na kiungo mshambuliaji, Miquissone kuwepo kikosini, Kocha Robertinho amekuwa na kigugumizi kwa kusema hata yeye hajui nani atakuwepo kikosini kesho ijapokuwa amesifu ubora wa Miquissone.

Advertisement
2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *