KOCHA Msiadizi wa Simba, Juma Mgunda amesema tayari wamekamilisha waandalizi ya mchezo wao dhidi ya Singida Big Star na ana matumaini watapata mazuri.
Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo amesema kuimarika kwa kikosi chao hasa usajili walioufanya kwenye dirisha dogo ndio vinampa matumaini ya kushinda mchezo huo ambao utachezwa Ijumaa wiki hii uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
“Tulishakamilisha maandalizi ya kuikabili Singida tunajua utakuwa mchezo mgumu kwa sababu tunakutana na timu yenye wachezaji wazuri na wamekuwa na matokeo mazuri katika mechi walizocheza hivi karibuni, lakini uhakika wa kuchukua pointi tatu ni mkubwa,”amesema Mgunda.
Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Liti, mkoani Singida zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.