Simba kazi imeanza upyaaa

DAR ES SALAAM: MENEJA Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ali amesema kuna kazi kubwa ya kupita tawi kwa tawi kurudisha hamasa kwa mashabiki wa Simba.

Ameyasema hayo katika Mkutano wake na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kuwakabili Asec Mimosas ya Ivory Coast katika hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Novemba 25, 2023 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

“Mechi hii ukisinzia tu unapata watu wachache uwanjani.

Mashabiki hamasa yao ipo chini. Niwaambie mashabiki, njoo na hasira zako, furaha utaikuta uwanjani,” amesema Ahmed Ali

Meneja huyo amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuiunga mkono timu yao, wakati huu uongozi ukiendelea kuimarisha benchi la ufundi kwa kusainisha makocha wenye viwango.

Kuelekea katika mchezo huo, Ali amesema kauli mbiu ni ‘Twendeni Kinyama (Kisimba simba), Mashabiki Bomba’.

Habari Zifananazo

Back to top button