Simba kuanzia Dar na Asec

AFRIKA KUSINI; Johannesburg. SIMBA itaanza kurusha karata zake hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa nyumbani kwa kumenyana na Asec Mimosas kutoka Ivory Coast Novemba 24 au 25, mwaka huu.

Desemba Mosi au 2, itakuwa ugenini ikimenya na Jwaneng huku Desemba 8 au 9 itakuwa Morocco ikimenya na Wydad Casablanca kabla ya kurudiana Desemba 18 au 19 kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es Salaam.

Kundi la Simba linatajwa kuwa na visasi kutokana na timu hizo zote kuwahi kukutana zaidi ya mara mbili.

Advertisement

Simba yupo Kundi B na vigogo Wydad Casablanca ya Morocco, Asec Mimosas kutoka Ivory Coast na Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Upinzani mkubwa utakuwa kati ya Simba na Wydad iliyowatoa kwenye Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Simba pia imepangwa na Jwaneng Galaxy iliyowatoa katika raundi ya kwanza tu Ligi ya Mabingwa msimu wa 2021/2022 kwa faida ya bao la ugenini baada ya kufungana mabao 3-3.

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *