KLABU ya Simba imesema hakuna mchezaji ambaye yupo kwenye mipango ya yao atakayeondoka msimu huu.
Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba, Ahmed Ally amesema uvumi wa Simba kuachia baadhi ya wachezaji msimu huu akiwemo Mohammed Hussein, Baleke na Manula hauna ukweli.
“Niwathibitishie wana Simba hakuna mchezaji ambaye yupo kwenye mipango yetu ataondoka.”amesema Ahmed Ally.
Ameongeza kuwa wachezaji waliomaliza mkataba ambao watatakiwa kuendelea watafanyiwa maboresho kwa lengo la kubaki nao.