Simba kuchuana na Al-Ahly michuano ya AFL.
SHIRIKISHO la Soka Afrika ( CAF) limetoa ratiba ya robo fainali ya michuano ya African Football League jioni hii.
Simba SC imepangwa kucheza na Al-Ahly ya Misri, baada ya michezo miwili, nyumbani na ugenini, atakayeshinda ataenda nusu fainali.
TP Mazembe ya DR Congo imepangwa kucheza dhidi ya Esperance.
Enyimba kutoka Nigeria, itachuana na Wydad ya Morocco. Petro Atletico itavaana na Mamelodi.