Simba kuendeleza ukuzaji vipaji

SIMBA SC inakusudia kuendeleza mfumo wa kukuza vipaji vya wachezaji vijana ili kuwa na uwanja mpana wa wachezaji wazuri na wenye vipaji.

Akizungumza na wanahabari leo Machi 23, 2023 Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Iman Kajula amesema mchakato huo hautainufaisha Simba pekee na taifa pia.

“Soka la vijana ni muhimu sana. Ili uwe na timu ya vijana iliyo bora lazima iwezeshwe. Kama ilivyo kwa wachezaji wengine kama Mohamed Hussein kutoka kwa timu ya vijana.” Amesema Kajula.

Advertisement

Kajula amesema mfumo huo utamwezesha kila kijana kukuza kipaji chake, lakini sio tu kuendeleza kipaji cha mpira lakini pia kusoma shule.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *