Simba SC imepangwa kukutana na mshindi kati ya African Stars ya Namibia na Power Dynamos ya Zambia kwenye Raundi ya Pili ya Mchujo wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL)
KLABU ya Yanga imepangwa kucheza na timu ya Asas Fc ya Djibout katika hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.
Mchezo wa kwanza unatarajiwa kupigwa kuanzia septemba 15-17, 2023, ambapo mshindi wa jumla kwenye mchezo huo atakutana na mshindi kati ya As otoho ya Congo ama El Merreikh ya Sudan.
Katika kombe la shirikisho barani Afrika timu ya Azam Fc imepangwa kucheza na Bahir Dar ya Ethiopia wakati Singida Fountain gate ikikipiga dhidi ya JKU ya Zanzibar katika hatua ya awali ya michuano hiyo.