Simba SC imepanga kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya CSKA Moscow inayoshiriki Ligi Kuu nchini Urusi.
CSKA Moscow ambayo mara kadhaa imekuwa ikishiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na michuano ya Ligi ya Europa, itacheza na Simba Januari 15, 2023 Dubai.
Simba inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki ikiwa mazoezini Dubai, Ijumaa Januari 13, 2023 dhidi ya Al Dhafrah ya Dubai.