Simba kuvuna Sh milioni 10 kila bao

Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa zawadi ya Sh 10 milioni kwa kila goli litakalofungwa katika mchezo wa African Football League kati ya Simba SC dhidi ya Al Ahly.

Mchezo huo wa ufunguzi utapigwa12:00 jioni dimba la Mkapa.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa ametoa taarifa hiyo alipozungumza na waandishi wa habari akiwa kata ya Mbagala, Wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam, ambako Simba wanaendelea na hamasa kuelekea mchezo huo.

“Kwenye michuano hii ya AFL, mheshimiwa Rais ameahidi, Simba katika kila mechi watakayoshinda, mechi watakayoshinda, kila goli moja, atatoa Sh milioni 10.” Amesema Msigwa.

Hatua hiyo ni muendelezo wa Rais Samia kuweka jitihada na hamasa kwenye michezo, kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo alikuwa akitoa Sh milioni 5-10 kwa kila bao lililofungwa na Simba SC na Yanga kwenye michuano ya CAF.

1 comments

Comments are closed.