Simba kuweka wazi hatima ya Mgunda

Juma Mgunda

UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema utaweka wazi hatima ya kocha wake msaidizi, Juma Mgunda baada ya kukamilika mazungumzo kati yao na kocha huyo.

Mgunda hajasafiri na kikosi cha Simba kilichokwenda kuweka kambi ya mwezi mmoja Uturuki kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara na michuano ya kimataifa msimu ujao.

Kutokuwemo kwenye msafara huo kwa kocha huyo kumezua sintofahamu juu ya hatima yake kwenye kikosi cha timu hiyo msimu ujao.

Advertisement

Lakini Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally aliliambia HabariLEO kuwa Mgunda amebaki Tanzania na hivi karibuni uongozi wa Simba utatoa taarifa rasmi kumhusu kocha huyo.

“Ni kweli Mgunda siyo sehemu ya msafara unaoondoka (leo) juzi kuelekea Uturuki, kuna mazungumzo anafanya na uongozi nadhani baada ya siku kadhaa uongozi utatoa taarifa yake rasmi,” alisema Ahmed ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuondoka nchini.

Gazeti hili limemtafuta Mgunda kutaka kujua kwa nini hakuongozana na timu nchini Uturuki, lakini kocha huyo alisema hana majibu na ni vyema ukaulizwa uongozi wa timu hiyo ndio wenye majibu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *