BAADA ya miaka 13 Simba SC imeagana na kiungo Jonas Mkude.
Simba imetangaza kuachana na Mkude kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, ikiwa ni mwendelezo wa kuachana na baadhi ya wachezaji ambao hawapo kwenye mipango ya timu msimu ujao.
“Tunamtakia kila la kheri kwenye changamoto mpya ya maisha ya soka nje ya Simba.
” Imeeleza taarifa hiyo.
Mpaka sasa Simba imechana na Mohamed Ouattara, Beno Kakolanya, Erasto Nyoni, Nelson Okwa, Victor Akpan na Jonas Mkude.