Simba Queens wafika kileleni

DAR ES SALAAM: TIMU ya wanawake ya SIMBA Queens imepanda hadi nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuizawadia pointi tatu na mabao matatu.
TFF imeeleza kuwa uamuzi huo umetokana na timu ya JKT Queens kukiuka kanuni ya 18:45 ya Ligi Kuu ya Wanawake toleo la 2023 kwa kushindwa kufika uwanjani katika mchezo namba 16 uliopanga kupigwa uwanja wa Azam Complex, Januari 09, 2024..

Simba Quees ambao walikuwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 19, sasa watasogea hadi nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 21.

Advertisement