Simba Queens yaendelea kugawa dozi Cecafa

SIMBA Queens imemaliza hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Ukanda wa Baraza la Vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) bila kufungwa baada ya kuifunga Yei Joints Stars mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Simba Queens imefikisha pointi tisa ikiwa kinara wa Kundi B ikifuatiwa na She Corporate ya Uganda yenye pointi sita baada ya kuifunga Garde Republicane ya Djibouti kwa mabao 8-0. Katika mchezo huo, Simba Queens ilianza kupata mabao yake dakika ya 13 kupitia kwa Vivian Corazone aliyeunganisha mpira wa kona iliyopigwa na nahodha Fatuma Issa ‘Fetty Densa’.

Dakika ya 21 iliongeza bao la pili lililofungwa na Philomena Abakah baada ya kupokea pasi ya Diana William na dakika ya 30 mshambuliaji, Opa Clement alifunga bao la tatu akipokea pasi ya Aisha Juma na dakika ya 64, Philomena tena alihitimisha karamu ya mabao.

Katika mchezo mwingine kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, She Corporate waliifunga Garde Republicane ya Djibouti kwa mabao 8-0 na kuungana na Simba Queens kufuzu nusu fainali baada ya kufikisha pointi sita.

Garde Republicane imeaga mashindano ikiwa imefungwa mabao 20-0 katika michezo mitatu na Yei Joints Stars inaondoka na pointi tatu ilifunga mabao sita na kufungwa mabao 10.

Michezo ya Kundi A, inatarajiwa kuendelea leo ambapo Commercial Bank FC ya Ethiopia itaivaa AS Kigali ya Rwanda na Fofila PF ya Burundi dhidi ya Warriors Queens ya Zanzibar.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x