Simba Queens, Yanga Princess patashika leo

Simba Queens, Yanga Princess patashika leo

#MICHEZO: Huku Opa Clement, kule Aniela Uwimana, kitaeleweka, Simba Queens itavaana na Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake utakaopigwa Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

Simba Queens inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza dhidi ya wapinzani wao bao 1-0 katika mchezo wa mwisho wa ligi.-

Advertisement

Kuelekea mchezo huo, makocha wa timu zote mbili wamezungumzia namna watakavyokabiliana na kuoneshana ufundi uwanjani.

“Kiufundi na kimfumo tutakuwa tunabadilika kutokana na hali itakavyokuwa lakini tumejipanga kuchukua pointi 3 dhidi ya Simba Queens,”  kocha wa Yanga, Princess Sebastian Nkoma.

“Itakuwa mechi ngumu, hii Derby na siku zote Simba ikikutana na Yanga inakuwa kama fainali. Tunafahamu Yanga ni timu nzuri na ina kocha mzuri pia lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Charles Lukula Kocha wa Simba Queens.