BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imebadilisha muda wa mchezo namba 119 wa Ligi Kuu Bara kati ya JKT Tanzania dhidi ya Simba SC kutoka saa 12:15 jioni hadi saa 10 jioni.
Katika taarifa iliyotolewa leo Februari 13 bodi hiyo imeutaarifu umma kuwa mchezo huo utachezwa Februari 15, 2024 Saa 10:00 Alasiri badala ya Saa 12:15 Jioni kama ilivyokuwa hapo awali.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa sababu ya mabadiliko hayo ni klabu ya JKT Tanzania FC kubadilisha uwanja wanaotumia katika michezo yao ya nyumbani kutoka Azam Complex kwenda uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo ambao hauna taa za kuwezesha kucheza majira ya usiku.