Simba SC kukamilisha malipo ya Teungueth

SIMBA SC imesema haikuwa na mawasiliano na klabu ya Teungueth ya Senegal hivyo kushindwa kumalizia deni lao lililotokana na kuuziwa kiungo Pape Ousmane Sakho.

Klabu hiyo imefikia uamuzi wa kutoa kauli hiyo kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA) kuifungia kwa kushindwa kulipa sehemu ya fedha za mauzo ya Sakho.

Kupitia taarifa ya Mtendaji Mkuu, Iman Kajula Simba imekiri na kupokea changamoto hiyo na kwamba iko mbioni kukamilisha malipo.

Advertisement

“Malipo ya awamu ya kwanza (50%) yalilipwa tarehe 2 October 2023 , Klabu ya Simba ilikuwa inasubiri awamu ya pili ili kuilipa asilimia 15% ya mauzo kwa klabu ya Teungueth ya Senegal”

“Klabu ya Simba itaendelea kuheshimu sheria, kanuni na kanuni na taratibu za mpira wa miguu kama ambavyo imekua ikifanya.” Imeeleza taarifa hiyo.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *