Simba SC kutumia uwanja wa Jamhuri

Simba wapo tayari kwa vita kesho

KLABU ya Simba SC itatumia Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro kuwa uwanja wake wa nyumbani kwa mechi za Ligi Kuu Bara.

Akizungumza kupitia mahojiano maalumu, Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amesema wataanza kutumia uwanja huo katika mchezo wao wa Machi 06, 2024 dhidi ya Tanzania Prisons.

“Kikosi kitaondoka kesho siku ya Jumanne kuelekea Morogoro. Jumatano Mungu akitufikisha na kutuamsha salama, tutaamkia Uwanja wa Jamhuri, tunakwenda kumnyonyoa mtu wetu, Tanzania Prisons,” ametamba Ahmed.

Advertisement

Kuelekea mchezo wao wa Jumatano, Ahmed amesema utakuwa mchezo mgumu, kwani Prisons wameimarika lakini hilo halitawazuia wao kuvuna alama tatu.

Hata hivyo amezungumzia hali ya kikosi hicho na kusema wachezaji wote wapo imara na kuhusu mshambuliaji wao Leandre Essomba Onana anaendelea vizuri.

“Kwa mujibu wa taarifa za madaktari wetu, huwenda akawa sehemu ya kikosi kitakachoanza siku ya Jumatano.” Amesema Meneja huyo.