Simba SC watua Ivory Coast kinyama

KIKOSI cha Simba SC kimewasili nchini Ivory Coast ambako watacheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Asec Mimosas.

Simba wameondoka jana usiku ambapo walipitia Addis Ababa, Ethiopia kisha kubadilisha ndege kuelekea Abdijan nchini humo.

Ijumaa hii, timu hiyo itakuwa ugenini nchini humo kuvaana na timu hiyo katika mchezo wa raundi ya nne ya michuano hiyo.

Advertisement

Katika mchezo wa awali uliopigwa Novemba 25, Simba iliambulia sare ya bao 1-1 uwanja wa Mkapa.

Msimamo wa kundi B, Asec anaongoza akiwa na pointi 10, Simba 5, Jwaneng 4, na Wydad pointi 3.