Simba SC yakamata usukani tena

SIMBA SC imerejea kileleni kwa mara nyingine tena, mara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Mabao ya Simba yamefungwa na Moses Phiri dakika ya 53 na 61 na Clatous Chama dakika ya 89.

Ushindi huo unaifanya Simba kuongoza ligi ikiwa na pointi 34, wakati Yanga wanaocheza kesho dhidi ya Tanzania Prison wakiwa nafasi ya pili na pointi 32, Azam FC, inashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 32 ambapo Jumatatu wanacheza na Polisi Tanzania.

Mabao mawili ya Phiri yanamfanya sasa kuwa na mabao sawa na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele (10)

Habari Zifananazo

Back to top button